logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Uchunguzi wa maiti wafichua sababu ya kifo cha mwanahabari wa NTV Rita Tinina

Akizungumza katika mochari ya Umash, msemaji wa familia Timothy Njaga alisema wameridhishwa na matokeo hayo.

image
na Samuel Maina

Habari19 March 2024 - 11:33

Muhtasari


  • •Akizungumza katika mochari ya Umash, msemaji wa familia Timothy Njaga alisema wameridhishwa na matokeo hayo.
  • •Pia alisema familia bado inaomba faragha na nafasi.
RITA TININA

Mwanahabari Rita Tinina alifariki kutokana na nimonia kali, uchunguzi wa maiti uliofanyika kwenye mwili wake umebaini.

Akizungumza katika mochari ya Umash Funeral Home, msemaji wa familia Timothy Njaga alisema wameridhishwa na matokeo hayo.

“Tulikuwa tumekuja hapa kushuhudia uchunguzi wa maiti na ukamilishwa na Dk Ndegwa na mwanapatholjioa wa familia. Tumepewa matokeo kuwa marehemu Rita alifariki kwa nimonia kali,” alisema.

Njaga alisema daktari wa mwanapathojia wa serikali Peter Ndegwa alifanya uchunguzi huo mbele ya mwanapathojia wa familia.

Pia alisema familia bado inaomba faragha na nafasi.

"Tunapaswa kukumbuka kuwa kuna familia ambayo imeathirika," Njaga alisema.

"Tunashukuru wanahabari kwa maneno yao mazuri kwa dada na rafiki yetu."

Baadhi ya wanahabari waliokuwepo wakati wa zoezi hilo ni pamoja na rais wa Chama cha Wahariri Kenya Zubeida Kananu na mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Bunge la Kenya Duncan Khaemba miongoni mwa wengine.

Rita Tinina alipatikana akiwa amefariki Jumapili katika nyumba yake Kileleshwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved