logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Murang'a: Jamaa aliyekuwa jela miaka 7 kwa mauaji aua wengine 2 baada ya kuachiliwa

Wanakijiji sasa wanaitaka serikali kuingilia kati na kumuondoa miongoni mwa jamii.

image
na Davis Ojiambo

Habari27 March 2024 - 12:55

Muhtasari


  • • Baada ya kumaliza kifungo na kurudi nyumbani, mwanamume huyo aliwaua kwa kuwacharanga mapanga wanaume wengine wawili kabla ya kuingia mitini.
Panga. Silaha ya muuajiiliyotumika

Wakaazi eneo la Mathioya kaunti ya Murang’a wamebaki na wasiwasi baada ya mwanamume ambaye alikuwa jela kwa miaka 7 kwa hatia ya mauaji kuua watu wengine wawili tena, miaka miwili baada ya kumaliza kifungo chake na kurudi nyumbani.

Kwa mujibu wa ripoti iliyopeperushwa kwenye runinga ya KBC, mwanamume huyo awali alikuwa amefungwa jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua wakongwe wawili.

Baada ya kumaliza kifungo na kurudi nyumbani, mwanamume huyo aliwaua kwa kuwacharanga mapanga wanaume wengine wawili kabla ya kuingia mitini.

Ripoti zinaonyesha kuwa alitenda mzaha na kuwakatakata Stanley Kamau Irungu na Benard Mahiu Mwangi (wote umri wa miaka 44) hadi kufa baada ya kutofautiana wakiwa katika baa ya eneo hilo.

Babake Kamau, Irungu Maina, alishindwa kuzuia machozi alipokuwa akisimulia jinsi kichwa cha mwanawe kilivyokuwa na michubuko mirefu, huku mwili wa marehemu ukiachwa ukiwa umelala njiani.

“Nina huzuni sana kwa sababu huyu ndugu yangu mdogo ndiyo tulikuwa tunasaidiana na yeye kwa mambo mengi, naomba serikali ijaribu imshike arudi jela,” alisema ndugu wa mmoja wa wanaume waliocharangwa mapanga.

Wakaazi hao waliokuwa na wasiwasi wa kutojua ni nani atakuwa mwathiriwa wa mshukuwa baadae, walitoa wito kwa serikali kupitia maafisa wake wa polisi kufanya msako na kumuondoa jamaa huyo miongoni mwa jamii wakimtaja kama tishio kwa maisha yao.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved