logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo ambayo yatakosa umeme leo, Alhamisi

KPLC ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti 11 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

image
na Radio Jambo

Burudani28 March 2024 - 03:56

Muhtasari


•KPLC ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti 11 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Kajiado, Uasin Gishu, Homa Bay, na Trans Nzoia, Bungoma, Kisii, Nyeri, Kwale, na Mombasa.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Machi 28.

Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti kumi na moja za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Kajiado, Uasin Gishu, Homa Bay, na Trans Nzoia, Bungoma, Kisii, Nyeri, Kwale, na Mombasa.

Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za eneo la South C, Kawangware, barabara ya Kikuyu na ya Naivasha zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu kadhaa za mji wa Limuru, Manguo, Ngarariga, Nyambare, soko ya Ruaka na Border Area katika kaunti ya Kiambu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Namanga, Bissil na mji wa Kajiado katika kaunti ya Kajiado zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Uasin Gishu, sehemu za maeneo ya Lingwai na Bindura zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kinyoro, Kaitet na Marambachi katika kaunti ya Trans Nzoia  pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Hongera Millers na Pan Paper Chemical katika kaunti ya Bungoma yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya Kanyamfwa, Nyamala na Otaro katika kaunti ya Homa Bay pia yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Sehemu ya mji wa Kisii katika kaunti ya Kisii pia itakosa umeme kati ya saa moja asubuhi na saa sita adhuhuri.

Katika kaunti ya Nyeri, maeneo ya Witima, Kagumo, Gaikundo, Mihuti na Mweru yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, wakaazi wa maeneo ya Tiwi, Kombani na Matuga katika kaunti ya Kwale pia wataosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Port Reitz na Migadini katika kaunti ya Mombaa pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved