KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Aprili 4.
Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Machakos,Migori, Nyeri, Embu, Kirinyaga, Kiambu, Busia, na Bomet.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za eneo la South C zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya mji wa Machakos, Athi River na Kangundo Road, Joska, Malaa katika kaunti ya Machakos zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Gogo na Rapogi katika kaunti ya Migori zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa nane alasiri.
Katika kaunti ya Nyeri, sehemu kadhaa za maeneo ya Blueline, Munyu, Kimahuri, Kiawambogo, Kianguru, Nyagatugu, Muthinga, Gichira, Kangaita na Wanjerere zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya soko ya Kianjiru na na Mururi na afisi ya gavana katika kaunti ya Kirinyaga zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Kivwe, Makengi, Kevote, Ena, Kithimu, na Rukira katika kaunti ya Embu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Sehemu za maeneo ya Thika Green na Gitingiri katika kaunti ya Kiambu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa saba mchana.
Katika kaunti ya Busia, baadhi ya sehemu za maeneo ya Nambale DC, Lugulu, Madende, Namahindi, na Mungatsi zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Chesilyot na Kaplong katika kaunti ya Bomet pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.