logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kizaazaa Mchina akirejea na kupata nyumba yake iliuzwa wakidhani alikufa kwa Corona (video)

Mchina huyo alisema aliondoka nchini 2016 na hakuweza kurudi kwa muda baada ya Corona kuzuka.

image
na Davis Ojiambo

Habari18 April 2024 - 14:20

Muhtasari


  • • Pia alieleza sababu nyingine iliyomzuia kurudi mapema ni pasipoti yake ya kusafiria kuisha muda wa matumizi, hivyo akalazimika kuanza upya mchakato wa kupata nyingine.
Mchina arudi na kupata nyumba imeuzwa

Kizaazaa kilishuhudiwa katika mji wa Mbeya jijini Tanzania baada ya mzee raia wa Uchina kurejea na kupata nyumba yake iliuzwa kitambo kwa kile alitaja kuwa walidhani alikufa kutokana na janga la Corona mapema 2020.

Kwa mujibu wa taarifa, nyumba yake iliuzwa na watu kwa shilingi milioni 80 za kitanzania, baada ya mzee huyo kwenda kwao Uchina na kukawia kurudi.

Mzee huyo alieleza aliondoka Tanzania mwaka 2016 kwa ajili ya shughuli za kifamilia lakini kabla hajarejea, janga la Covid-19 likabisha.

Hapo ndipo alilazimika kuongeza kipindi cha kukaa kwao Uchina kwani kusafiri kulipigwa marufuku kama njia moja ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Pia alieleza sababu nyingine iliyomzuia kurudi mapema ni pasipoti yake ya kusafiria kuisha muda wa matumizi, hivyo akalazimika kuanza upya mchakato wa kupata nyingine.

Baada ya kufanikisha michakato yote na kurejea Aprili 2024, alipigwa na butwaa kupata nyumba yake iko chini ya umiliki mpya, akiambiwa kwamba iliuzwa wakidhani aliangamia kwa Corona.

“Mimi 2016 nilienda China, huko Corona ikafunga, hamna kusafiri, baadae ikafunguliwa na nikapata pasipoti nyingine nikaja, kufika huku nikapata tayari nyumba yote imeuzwa, wakisema nilienda China nikafa kwa Corona, wakasema haraka uza nyumba,” Mchina huyo alibananga kiswahili.

Tazama video ya kisa hicho cha kushangaza hapa;

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved