Joel Rabuku Ogolla, mtoto wa marehemu Mkuu wa Majeshi Jenerali Francis Ogolla, amepuuzilia mbali tetesi za uhusiano wowote mbaya kati ya babake na rais William Ruto.
Wakati akiwahutubia waombolezaji waliokusanyika kwa ajili ya mazishi ya babake katika eneo la Nginya, Kaunti ya Siaya, Joel alibainisha kuwa kumekuwa na uvumi mwingi kuhusu hali ya uhusiano mzazi huyo wake na viongozi wa taifa.
Hata hivyo aliweka wazi kuwa marehemu jenerali Ogolla alikuwa na uhusiano mzuri wa kikazi na muungano mzuri na rais Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua. Alidokeza kuwa rais alimteua babake kutokana na sifa zake.
“Rais hakupaswa kumteua kwanza, na awali aliona sifa zake na akaona huyu ndiye mtu sahihi wa kazi hiyo.
Lakini haraka sana walianza kuwa marafiki na wakaunda muungano mzuri ambao angeniambia ‘nimekuwa na mkutano mzuri sana na bosi’,” alisema.
Aliongeza, "Si yeye tu, na naibu rais pia. Walifurahia sana kuwa naye na walikuwa na uhusiano mkubwa wa usalama wa kupata nchi. Mawaziri wake wakawa kama ndugu zake.”
Kijana huyo alidokeza kwamba alizungumza na baba yake mara kwa mara na angemhakikishia kuhusu uhusiano mzuri wa kikazi aliokuwa nao na viongozi wa nchi.
Pia alipuuzilia mbali madai ya rais Ruto kughushi machozi wakati wa ibada ya kumbukumbu ya marehemu Francis Ogolla jijini Nairobi mnamo Jumamosi.
"Moyoni mwangu najua ilikuwa kweli," alisema.
Aidha, Omondi aliwakashifu wanablogu kwa kutojali watu wanaopitia nyakati ngumu.
“Kuna wanablogu wasio na maana, ambao ni wepesi wa kuweka picha. Watu wengine hawana hisia. Kwa hiyo umetoa habari, umepewa kazi yake?” alihoji..
Ogolla alikuwa miongoni mwa maafisa 10 wa jeshi waliofariki katika ajali ya helikopta Alhamisi kwenye mpaka kati ya kaunti za Elgeyo Marakwet na Uasin Gichu.
Walikuwa kwenye misheni ya amani katika eneo lenye mizozo la Bonde la Ufa, ambalo limekuwa likikumbwa na wizi wa mifugo na ujambazi.