Aliyekuwa waziri wa fedha Ukur Yattani amekamatwa
Kukamatwa kwake kunajiri baada ya maafisa wa upelelezi kutoka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kufanya msako mkali katika nyumba yake na ya Gavana wa Marsabit Mohamud Ali.
Uvamizi huo ulifanyika katika nyumba zao za Nairobi na Marsabit.
Yattani aliwahi kuwa gavana wa Marsabit kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta.
Nyumba za maafisa wakuu kutoka kaunti hiyo pia zilivamiwa.
EACC iliithibitishia Star kwamba Gavana huyo wa zamani yuko chini ya ulinzi wao na atapelekwa katika Kituo cha Uadilifu.
Maelezo mengine kufuata...