logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania yaonya kuhusu mvua kubwa

Mgandamizo mdogo wa hewa unatarajiwa kutawala na kusababisha mvua kubwa na upepo mkali katika mikoa mitano nchini humo.

image
na Samuel Maina

Habari02 May 2024 - 05:46

Muhtasari


  • •Mgandamizo mdogo wa hewa unatarajiwa kutawala na kusababisha mvua kubwa na upepo mkali katika mikoa mitano nchini humo.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania TMA imatangaza kuwepo kwa mgandamizo mdogo wa hewa ambao unatarajiwa kutawala na kusababisha mvua kubwa na upepo mkali katika mikoa mitano nchini humo.

Mgandamizo huo unatarajiwa kuimarika na kufikia hadhi ya kimbunga kamili kufikia leo tarehe 2 mwezi Mei 2024,

‘’Hali hiyo inatarajiwa kusogea na kuelekea baadhi ya maeneo ya pwani ya nchi yetu kuanzia usiku wa kuamkia siku ya Ijumaa tarehe 3 mwezi Mei 2024’’, ilisema TMA katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kuathiriwa na mvua hiyo pamoja na upepo ni mikoa ya Mtawara , Lindi, Pwani, Morogoro ,Dar es salaam na maeneo Jirani.

Serikali imewashauri wananchi kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri wa hali ya hewa ili kupata ushauri na mwongozo wa wataalam katika sekta husika kwa lengo la kujikinga na athari zinazoweza kuibuka.

Mamlaka ya hali ya hewa hatahivyo imesema mgandamizo huo mdogo unatarajiwa kupungua nguvu baada ya tarehe 6 Mei 2024.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved