logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamume aokolewa siku tano baada ya jumba kuporomoka

Watu 81 walikuwa wakifanya kazi kwenye mjengo huo wakati wa ajali hiyo

image
na Radio Jambo

Habari12 May 2024 - 06:00

Muhtasari


  • Waokoaji walifanikiwa kuwasiliana na mwanamume huyo na kumpa maji ya kunywa baada ya kumsikia akiwa chini ya vifusi.

Mfanyakazi ameokolewa kwenye vifusi vya jumba kuporomoka kwenye mji wa George Afrika Kusini. Mwanamume huyo alikuwa amekwama kwa siku tano.

Waokoaji walifanikiwa kuwasiliana na mwanamume huyo na kumpa maji ya kunywa baada ya kumsikia akiwa chini ya vifusi.

Kiongozi wa jimbo la Western Cape Alan Winde amesema kwamba uokoaji huo ulikuwa muujiza waliokuwa wakiutarajia.

Jumba hilo ambalo lilikuwa limekamilika ujenzi kwa upande mmoja huku mwingine ukiendelea kujengwa – uliokuwa makaiz ya watu – uliporomoka jumatatu na kusababisha vifo vya watu 14 huku wengine 39 wakiwa hawajulikani waliko.

Watu 81 walikuwa wakifanya kazi kwenye mjengo huo wakati wa ajali hiyo, kwa mujibu wa taarifa ya usimamizi wa mji huo. 13 ya waliookolewa wanapokea matibabu hospitalini.

Kituo cha Habari cha News24 kimeripoti kwamba mwanamume aliyookolewa ametambuliwa kama Gabriel Gambe , mwenye 33 ambaye ni fundi ujenzi ambaye alionekana akibebwa kwa ambulensi.

Uokoaji wa hivi punde unafuatia mwingine wa Delvin Safels mwenye umri wa miaka 29 aliyeondolewa kwenye vifusi jumatano Mei 8 . Uokozi wake uliwavutia wengi baada ya yeye kuwatumia familia yake ujumbe wa sauti mara kwa mara kwamba anawapenda na akiwa mwenye hofu kwamba hataokolewa.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved