Mwanamke mmoja amedai kuwa alikuwa akishiriki mapenzi kila usiku na mzimu 'mwenye meno refu na uso wa gargoyle' kwa zaidi ya miaka 20.
Paula Flórez, kutoka Colombia, alisema uhusiano wake na roho hiyo ulianza alipokuwa mdogo - na kwamba mzimu huyo mwenye hasira alimtembelea kila usiku alipokuwa amelala.
Alitoa madai hayo kwenye kipindi cha Runinga cha Sin Carreta, kinachopeperusha matangazo kwenye chaneli inayomilikiwa na serikali cha Canal 1, Daily Mail la Uingereza lilieleza.
Paula pia alidai kuwa alianzisha kila mara na kwamba aliishia kumpenda mtu huyo mwenye mvuto, hata kufurahia kushiriki naye kimapenzi kwa miaka 20.
Aliwaambia watazamaji: 'Siku moja, nilikuwa nimelala niliposikia mkono ukisogezwa kutoka miguuni mwangu hadi kifuani. Ilikuwa ya ajabu, niliogopa. Kuanzia wakati huo na kuendelea, alianza kuja kwangu kama mzimu kufanya mapenzi nami.'
Paula alijiona kama mshirika mwenye upendo kwa mpenzi wake wa kiroho kwa miaka 20 - hadi hatimaye alipouona uso wake.
Alieleza: 'Alikuwa mtu mkubwa sana. Lakini siku nilipomwona, alikuwa na meno refu na uso wa gargoyle'.
Baada ya kuona sura ya kutisha ya ghoul, alisema kwamba hakutaka kuwasiliana naye tena kwa sababu alimuogopa.
Mwanamke huyo aliendelea: 'Mara ya mwisho nilipoona uso wake ndio wakati ambapo sikutaka kuendelea naye tena kwenye mapenzi.'
Je, unamini katika mizimi kuwatokea watu walio hai?