logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Haiti yapata waziri mkuu mpya huku taifa hilo likiendelea kuzingirwa na magenge ya wahalifu

Garry Conille ameteuliwa kama waziri mkuu nchini Haiti na baraza la watu sita baada ya Ariel Henry kujiuzulu.

image
na Davis Ojiambo

Habari29 May 2024 - 06:29

Muhtasari


  • •Wajumbe sita kati ya saba walio na mamlaka ya kupiga kura walimchagua Conille mapema Jumanne 28,2024
  • •Mbali na kuchagua waziri mkuu mpya, baraza hilo pia lina jukumu la kuchagua Baraza jipya la Mawaziri na kufanya uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka ujao.
Picha:Hisani

Garry Conille aliteuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Haiti Jumanne jioni,takriban mwezi mmoja baada ya muungano ndani ya baraza la mpito lililovunjika kuchagua mtu mwingine kwa nafasi hiyo.

Hatua hiyo iliyosubiriwa kwa muda mrefu inakuja huku vikosi vya uhalifu vikiendelea kuutia hofu mji mkuu wa Port-au-Prince, wakifyatua risasi katika vitongoji vilivyokuwa na amani na kutumia mashine nzito kubomoa vituo kadhaa vya polisi na magereza.

Mwanachama wa baraza hilo Louis Gérald Gilles aliambia 'The Associated Press' kwamba wajumbe sita kati ya saba walio na mamlaka ya kupiga kura walimchagua Conille mapema Jumanne.Mwanachama mmoja,Laurent St. Cyr, hakuwepo nchini Haiti na hivyo hakupiga kura.

Conille, ambaye ni mkurugenzi wa kanda wa UNICEF kwa Amerika ya Kusini,aliwahi kuwa waziri mkuu wa Haiti kuanzia Oktoba 2011 hadi Mei 2012 chini ya Rais wa wakati huo Michel Martelly. Conille anachukua nafasi ya Michel Patrick Boisvert, ambaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa muda baada ya Ariel Henry kujiuzulu kupitia barua mwishoni mwa mwezi Aprili.

Henry alikuwa katika safari rasmi nchini Kenya wakati muungano wa magenge yenye nguvu ulipoanzisha mashambulizi yaliyoratibiwa Februari 29, na kutwaa udhibiti wa vituo vya polisi, kufyatua risasi katika uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa wa Haiti na kuvamia magereza makubwa mawili ya nchi hiyo,na kuwaachilia wafungwa zaidi ya 4,000.

Henry alifungiwa nje ya nchi kutokana na mashambulizi hayo, huku uwanja wa ndege katika mji mkuu wa Port-au-Prince ukisalia kufungwa kwa karibu miezi mitatu.

Vikosi vya uhalifu bado vinaendelea kuvuruga  katika sehemu za mji mkuu wa Haiti na kwingineko huku Conille akichukua usukani wa nchi hiyo yenye matatizo,akisubiri kutumwa kwa jeshi la polisi kutoka Kenya na nchi nyingine zinazoungwa mkono na umoja wa mataifa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved