KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Julai 4.
Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Makueni, Kiambu, Nyeri, Kirinyaga, na Busia.
Katika kaunti ya Nairobi, eneo la Village Market litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Emali na Sultan katika kaunti ya Makueni zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Murera Sisal na Juja Farm katika kaunti ya Kiambu zitashuhudia kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Nyeri, sehemu kadhaa za maeneo ya Ithenguru na Kiandu zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na mbili asubuhi.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kutus na Kagio katika kaunti ya Kirinyaga pia zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu na saa tisa unusu alasiri.
Eneo la Mau Mau Market katika kaunti ya Busia pia litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na mbili asubuhi.