KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Julai 10.
Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Embu, Meru, Nyeri, Nakuru, Siaya, na Isiolo.
Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za maeneo ya Kasarani Seasons na Runda Mimosa zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Masinga na Ekalakala katika kaunti ya Embu zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za eneo la Kongo Acheke katika kaunti ya Meru pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Nyeri, sehemu za maeneo ya Kamatogu, Watuka, na shule ya upili ya Kirimara zitashuhudia kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Barnabas na Mbaruk katika kaunti ya Nakuru pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Mbaga na Hawinga katika kaunti ya Siaya zitashuhudia kukatizwa kwa umeme katu ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Eneo la Asili Millers katika kaunti ya Isiolo pia litakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.