logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Burkina Faso kuharamisha mapenzi ya jinsi moja

Uganda ilipitisha mojawapo ya sheria kali zaidi duniani dhidi ya LGBTQ mwezi Mei mwaka jana.

image
na Radio Jambo

Habari11 July 2024 - 13:04

Muhtasari


  • Wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri, serikali inayoongozwa na jeshi iliidhinisha sheria inayopiga marufuku ndoa za mapenzi ya jinsi moja na mila kama hiyo.
Mwanaharakati akipeperusha bendera ya kujivunia mashoga wakati wa maandamano huko Nairobi. Picha: MAKTABA

Burkina Faso imekuwa nchi ya hivi punde zaidi barani Afrika kuharamisha mapenzi ya jinsi moja.

Wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri, serikali inayoongozwa na jeshi iliidhinisha sheria inayopiga marufuku ndoa za mapenzi ya jinsi moja na mila kama hiyo.

Waziri wa sheria wa Burkina Faso Edasso Rodrigue Bayala amesema sheria hiyo mpya inatambua ndoa za kimila na kidini pekee chini ya sajili yake ya kiraia.

Sheria hiyo sasa itaendelea ili kuidhinishwa na bunge kabla ya kutiwa saini na Ibrahim Traore - kiongozi wa mapinduzi ambaye alisimamia mkutano wa baraza la mawaziri.

Taifa hilo la Afrika Magharibi lilikuwa miongoni mwa nchi ishirini na mbili kati ya hamsini na nne zilizoruhusu mapenzi ya jinsi moja ambayo yanaadhibiwa kwa kifo au kifungo cha muda mrefu jela kwa nchi nyingine.

Uganda ilipitisha mojawapo ya sheria kali zaidi duniani dhidi ya LGBTQ mwezi Mei mwaka jana.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved