Marekani imewashauri raia wake kuepuka Barabara kuu ya A104 iliyopo katika eneo la Kambembe Rironi, Kaunti ya Kiambu, kufuatia kumwagika hatari kwa Sodium Cyanide baada ya lori iliyokuwa ikiisafirisha kupinduka.
Tukio hilo la Jumamosi liliibua wasiwasi wa usalama kutokana na sumu kali ya kemikali hiyo.
Ubalozi wa Marekani nchini Kenya unawashauri raia wake kutumia barabara ya Limuru kama njia mbadala kuepuka Westlands (barabara ya Waiyaki) na taarifa zaidi kuhusu usalama wa eneo lililoathiriwa.
Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi kufuatia ajali hiyo ya lori, Wizara ya Afya pia ilitahadharisha kuwa sodium cyanide ina sumu kali na inaweza kusababisha kifo kwa kiasi kidogo ikiwa itamezwa au kuvutwa kwa njia ya pumzi.