logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Ikiwa hufai, tutakutupa nje,' Junet Mohammed kwa mawaziri walioteuliwa

Jukumu la kuidhinisha au kutoidhinisha mawaziri walioteuliwa  liko mikononi mwa kamati

image

Habari23 July 2024 - 15:12

Muhtasari


  • Akiongea Jumanne katika Bunge la Kitaifa, Junet, ambaye ni mmoja wa wanakamati ya uhakiki, alidokeza mchujo wa kina ambao unasubiri mawaziri hao walioteuliwa.

Kinara wa Walio wachache katika Bunge la Kitaifa Junet Mohammed ametuma onyo kwa baadhi ya  Mawaziri walioteuliwa na Rais William Ruto.

Akiongea Jumanne katika Bunge la Kitaifa, Junet, ambaye ni mmoja wa wanakamati ya uhakiki, alidokeza mchujo wa kina ambao unasubiri mawaziri hao walioteuliwa.

"Nataka kuwaambia wanachama kuwa hii haitakuwa biashara kama kawaida, kama mtu hafai, hawezi, au hana uwezo, tutamtupa nje."

Mbunge huyo wa Suna Mashariki alibainisha kuwa kamati hiyo iliapa kuona kuwa uchunguzi wa kina na uhakiki unafanywa kwa walioteuliwa kwa heshima ya vijana waliovamia barabarani kuandamana na kushinikiza mageuzi na marekebisho ya serikali.

Akitoa dokezo la baadhi ya mambo ya kuzingatia, Mbunge huyo alisema watazingatia thamani ya kila mteule, huku akisisitiza kuwa watamkataa mtu yeyote ambaye rekodi yake ya thamani yake haitaendana na mshahara wa mwezi.

Jukumu la kuidhinisha au kutoidhinisha mawaziri walioteuliwa  liko mikononi mwa kamati ya kuhakiki Bunge la Kitaifa baada ya Rais Ruto kuteua kundi la kwanza la Makatibu wa Baraza la Mawaziri.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved