Rais William Ruto adhuhuri ya Jumatano aliteua kundi la pindi la baraza lake la mawaziri.
Akizungumza na wanahabari kutoka ikulu ya Nairobi, kiongozi wa nchi aliteuwa kundi la watu wengine 10 ambao watajiunga na wenzao 11 ambao waliteuliwa mwishoni mwa juma lililopita ili kuunda baraza kamilifu la mawaziri.
Hata hivyo, kaitka baraza hilo, baadhi ya majina kutoka kwa wanachama wa upinzani yalitajwa na watakuwa wanasubiria kupitia mchujo katika bunge la kitaifa kabla ya kuapishwa kama mawaziri.
Hawa hapa ni baadhi ya watu kutoka mrengo wa upinzani ambao wameteuliwa katika serikali ya Kenya Kwanza kama mawaziri.
Aliyekuwa mbunge wa Mombasa Hassan Joho aliteuliwa kama waziri wa madini na uchumi wa baharini, mbunge mteule John Mbadi akiteuliwa kama waziri wa fedha.
Aliyekuwa gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya atatarajiwa kuongoza wizara ya Vyama vya Ushirika na SMEs, kiongozi wa wachache katika bunge la Kitaifa Opiyo Wandayi akiteuliwa kama waziri wa nishati.
la mawaziri
John mbadi – fedha
Opiyo wandayi – nishati
HASSAN Joho – madini na uchumi wa baharini
Oparanya – SMEs