logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DRC na Rwanda wakubaliana kuhusu amani

Rwanda na DRC, walisema kuwa tukio hilo litadhibitiwa na chombo cha pamoja cha ufuatiliaji wa masuala ya usalama kati ya Rwanda na Congo.

image
na SAMUEL MAINA

Habari01 August 2024 - 03:51

Muhtasari


  • •Rwanda na DRC, walisema kuwa tukio hilo litadhibitiwa na chombo cha pamoja cha ufuatiliaji wa masuala ya usalama kati ya Rwanda na Congo.
Mawaziri Thérèse Kayikwamba (kushoto) na Olivier Nduhungirehe (kulia) wakiwa na Tete Antonio kati yao.

Katika mkutano wa kwanza uliowaleta pamoja mawaziri wa mambo ya nje wa DR Congo na Rwanda, viongozi hao wamekubaliana kuhusu makubaliano ya amani "kati ya pande zinazozozana mashariki mwa DRC" ambayo yataanza kutekeleza Jumapili tarehe 04 mwezi ujao wa Agosti.

Ni uamuzi uliotolewa katika kikao kilichofanyika Luanda, Angola Jumanne kati ya Thérèse Kayikwamba Wagner upande wa Kongo na Olivier Nduhungirehe wa Rwanda, akiungana na mwenzao Tete Antonio wa Angola.

Katika matangazo yaliyochapishwa na wizara za pande zote mbili, Rwanda na DRC, walisema kuwa tukio hilo litadhibitiwa na chombo cha pamoja cha ufuatiliaji wa masuala ya usalama kati ya Rwanda na Congo.

Rwanda inasema kuwa "bado inaendelea kuwa na nia ya kufikia amani ya kudumu katika eneo hilo kwa kutatua vyanzo vya mzozo huu".

Congo inaishutumu Rwanda kwa kuwasaidia wapiganaji wa M23, na Rais Félix Tshisekedi aliendelea kusema kwamba hatazungumza na M23, akisema kwamba Rwanda iko nyuma yake. Rwanda inakana shutuma hizo


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved