KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Julai 25.
Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nakuru, Kiambu, Nyamira, Kisii, Nyeri, Kirinyaga, Siaya, na Mombasa.
Katika kaunti ya Kiambu, sehemu za maeneo ya Gitaru na Regen zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Ngata, Ogilgei, na Piave katika kaunti ya Nakuru yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.
Maeneo ya Nyankoba na Birongo katika kaunti ya Nyamira pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Katika kaunti ya Kisii, eneo la kiwanda cha chai cha Eberege litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Eneo la Karima Mission School katika kaunti ya Nyeri litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Katika kaunti ya Kirinyaga, maeneo ya Gitwe na Kona Mbaya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Maeneo ya Nango, Wagusum, na Sirongo katika kaunti ya Siaya yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za eneo la Shanzu katika kaunti ya Mombasa zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.