Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kimetangaza kufutilia mbali uteuzi wa Cleophas Malala kama Katibu Mkuu wa muda.
Katika taarifa yake siku ya Ijumaa, chama hicho kilisema kwamba baada ya kushauriana, nafasi hiyo itachukuliwa na makamu mwenyekiti, Hassan Omar, kwa muda.
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho imesema mabadiliko hayo yanaanza mara moja.
“Baada ya majadiliano mapana na ya mashauriano, kwa kuzingatia na kwa mujibu wa mamlaka yake chini ya Ibara ya 8.2 ya Katiba ya Chama, Halmashauri Kuu ya Taifa imeazimia kumteua Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa Hassan Omar Hassan kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu kwa muda.
"Uteuzi wa Mhe Cleophas Malala kuwa Katibu Mkuu wa muda unafutiliwa mbali," chama kilisema.