logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tazama maeneo ambayo yatakosa stima leo, Alhamisi - KPLC

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Meru, Laikipia, na Nyeri.

image
na Samuel Maina

Habari22 August 2024 - 04:20

Muhtasari


  • •KPLC imesema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Meru, Laikipia, na Nyeri.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Agosti 22. 

Katika taarifa ya Jumatano, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Meru, Laikipia, na Nyeri.

Katika kaunti ya Meru, sehemu za maeneo ya Mikinduri na Kigucwa zitakosa umeme kati ya  saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Makutano na Kongoni  katika kaunti ya Laikipia yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.

Wakazi wa mji wa Othaya na Mahiga katika kaunti ya Nyeri pia watashuhudia kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved