Spika wa bunge la seneti Amason Kingi amewasihi maseneta kutumia fursa wanayopewa kuuliza maswali vyema na wala si kutumia nafasi hiyo kufanya utani ili video zisambae kwenye mtandao wa tik tok.
Kingi amesema hayo wakati wa kikao ambapo maseneta wanajadili hoja ya kumtimua naibu wa rais Rigathi Gachagua kutoka mamlakani, hoja iliyowasilishwa bungeni humo baada ya bunge la kitaifa kuidhinisha kubanduliwa kwake.
“Wakati umepewa nafasi ya kutaka ufafanuzi ama kuuliza swali, si wakati wa kupata video ya kuchapisha kwenye mtandao wa tik tok.” Alisema spika Kingi.
Mwenyekiti huyo anayeongoza kusikilizwa kwa madai yaliyowasilishwa na mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse, amewarai maseneta kutoaibisha bunge la seneti katika vikao hivyo muhimu vilivyoanza Jumatano 16.
Maseneta wamefanya kikao kwa siku ya pili wakijadili kuhenguliwa kwa naibu wa rais ambapo wamekuwa wakihakiki maswala yaliyoibuliwa na mwasilishaji wa hoja hiyo na mawakili wa naibu wa rais.
Hatma ya
kubanduliwa kwa Gachagua ipo mikononi mwa maseneta wanaotarajiwa kutoa uamuzi
Alhamisi 17, ikiwa atabanduliwa.