Mfuasi
maarufu wa ODM na kinara wa chama hicho Raila Odinga, Nuru Okanga alishindwa
kuficha furaha yake siku ya Ijumaa jioni wakati akisherehekea kuondolewa
madarakani kwa naibu rais Rigathi Gachagua.
Okanga ambaye ni mwanachama maarufu wa kikao maarufu cha Bunge la Mwananchi kinachofanyika katika Kiwanja cha Jacaranda, jijini Nairobi alisimulia furaha yake kwa wanachama wenzake na watazamaji huku akibainisha kuwa Gachagua hakufaa kushikilia kiti hicho.
Alibainisha
kuwa alifurahishwa sana na hatua ya bunge na seneti kumtimua Gachagua, kiasi
kwamba alikuwa tayari kuvua nguo zake ili kudhihirisha hilo.
“Wacha
nitoe nguo Gachagua, Gachagua, Gachagua!!” Nuru Okanga alifoka kabla ya kuvua
suruali yake.
“Gachagua
ameenda nyumbani*2, Mimi nilisema lazima Wakenya wajue Gachagua ameenda
nyumbani,” aliendelea kusema huku suruali yake ikiwa chini kwenye miguu yake.
Mfuasi huyo sugu wa chama cha ODM aliendelea kueleza kuwa hakufurahishwa na mtazamo wa Gachagua kuhusu jinsi nchi inavyofaa kuongozwa.
“Mimi
niko na furaha kwa sababu tumempeleka Mathira mtu ambaye amesema Kenya ni
kampuni. Kumbe Bondo ni karibu kuliko Mathira, Gachagua*3 mambo yake imeisha,”
alisema.
Haya yalijiri kufuatia kuondolewa madarakani kwa naibu rais Rigathi Gachagua na seneti, na kuteuliwa kwa naibu rais mpya Kindiki Kithure na rais William Ruto.
Maseneta wengi mnamo Alhamisi usiku waliunga mkono kuondolewa kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua licha ya upande wa utetezi kuonekana kufanya vizuri katika kazi yao..
Maseneta waliidhinisha mashtaka matano kati ya 11 yaliyotolewa dhidi ya Gachagua.
"Seneti imeazimia kumuondoa afisini kwa kumwondoa madarakani MHE. Rigathi Gachagua, Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya. Kwa hiyo, H.E. Rigathi Gachagua akoma kushikilia wadhifa huo,” Spika Amason Kingi alisema.
Mashtaka yaliyoidhinishwa ni pamoja na; shtaka la maoni ya Wanahisa, mashtaka manne ya kuingilia Uhuru wa Majaji na mashtaka matano ya Sheria ya Uwiano na Uadilifu wa Kitaifa.
Pia walishikilia misingi ya sita na tisa kuhusu uhalifu chini ya Sheria ya Uwiano wa Kitaifa na Utovu wa Maadili Mkubwa.