logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Familia kadhaa zahofiwa kukwama baada ya jengo la ghorofa kuporomoka Kahawa West

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema kuwa timu imetumwa kusaidia shughuli ya uokoaji.

image
na SAMUEL MAINAjournalist

Habari20 October 2024 - 13:10

Muhtasari


  • Jengo la orofa nyingi lenye nyumba za makazi na biashara kadhaa limeripotiwa kuporomoka katika eneo la Kahawa West, Nairobi  siku ya Jumapili adhuhuri.

Jengo la orofa nyingi lenye nyumba za makazi na biashara kadhaa limeripotiwa kuporomoka katika eneo la Kahawa West, Nairobi  siku ya Jumapili adhuhuri.

Familia kadhaa zinahofiwa kukwama ndani ya jengo hilo ambalo kuanguka kwake kulirekodiwa katika video zinazovuma kwenye mitandao ya kijamii.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema kuwa timu imetumwa kusaidia shughuli ya uokoaji.

"Timu ya mashirika mengi ya kukabiliana na matukio kwa sasa inajibu kufuatia kuporomoka kwa jengo katika eneo la Kahawa Magharibi, Kaunti ya Nairobi, ambapo watu wanahofiwa kunaswa." Msalaba Mwekundu alisema katika taarifa.

Taarifa zaidi zitafuata punde tutakapozipata...



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved