logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Meneja wa Wells Fargo, Willis Ayieko aling’olewa macho, kukatwa maskio kabla ya kuibiwa bastola yake

Pia walimng'oa macho, wakakata masikio yake na kuuburuta mwili wake kwenye ardhi.

image
na Davis Ojiambo

Habari24 October 2024 - 16:28

Muhtasari


  • Aliondoka jijini mwendo wa saa moja jioni siku ya Ijumaa lakini hakurudi nyumbani, jambo lililozua wasiwasi kuhusu aliko.
  • Rafikize walisema Ayieko alitarajiwa kuhudhuria hafla nyingine mjini Kakamega siku ya Jumamosi, Oktoba 19, lakini hakufika.

Wauaji wa meneja wa wafanyikiza wa Wells Fargo ambaye mwili wake ulipatikana mtoni huko Yala, Kaunti ya Siaya waliiba bastola yake.

Pia walimng'oa macho, wakakata masikio yake na kuuburuta mwili wake kwenye ardhi.

Jamaa wa familia yake Willis Ayieko waliouona mwili huo muda mfupi baada ya kupatikana walisema wauaji hao pia walimtesa kabla ya kumuua.

"Mauaji hayo yalikuwa ya kikatili kwa sababu waliondoa macho yake, wakamkata masikio na kumpiga tumboni na usoni," kaka yake alisema.

Mwili huo uligunduliwa katika mto wa Mungowere huko Yala, Kaunti ya Siaya mnamo Oktoba 23 saa mbili usiku.

Ayieko, 55 alikuwa mmiliki wa bunduki aliyeidhinishwa, Afisa wa Uchunguzi wa Jinai wa Kanda ya Nyanza Lenny Kisaka alisema.

Maafisa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na Uwanja wa Ndege wa Kisumu walisema alipoondoka na kufika, alikuwa amejihami kwa bastola iliyokuwa na risasi 14.

Familia yake ilikuwa imeripoti kuwa alitoweka Jumatatu, Oktoba 21.

Polisi walisema mwili huo ulikuwa umeoza wakati mwanafunzi aliugundua. ulikuwa na michubuko usoni na tumboni kuashiria ulikuwa umeburutwa kwenye sehemu mbaya.

Sababu ya mauaji hayo bado haijajulikana. Kikosi cha wapelelezi wa mauaji kutoka makao makuu ya DCI waliungana na wale waliokuwa nyanjani siku ya Alhamisi kufuatilia mauaji hayo.

Kisaka alisema mwili huo uligunduliwa kilomita chache kutoka ambapo gari la Ayieko lilipatikana likiwa limetelekezwa.

Mwili huo ulikuwa nusu uchi na ulionekana kuteswa sehemu nyingine kabla ya kutupwa eneo la tukio. Kisha wauaji hao waliendesha gari lake hadi eneo la Sabatia ambalo liko umbali wa kilomita chache na kulitelekeza kando ya barabara.

Ayieko alitoweka Ijumaa iliyopita Oktoba 18 baada ya kuhudhuria hafla ya mazishi huko Gem, Kaunti ya Siaya.

Alikuwa amekaa hadi saa 10 jioni kabla ya kuondoka kwenye mazishi bila kupatikana akiwa hai.

Polisi wanasema kanda za CCTV zilinasa wanaume wawili wakiacha gari la Ayieko karibu na kituo cha mafuta huko Sabatia.

Wachunguzi wanatumai kuwatambua watu hao ili kutoa taarifa muhimu kuhusu jinsi walivyopata gari hilo.

Haijabainika kwa nini Ayieko alilengwa. Kikosi cha wapelelezi kilitembelea maeneo mbalimbali ambayo gari lilipita kama sehemu ya uchunguzi wa mauaji hayo.

Aliondoka jijini mwendo wa saa moja jioni siku ya Ijumaa lakini hakurudi nyumbani, jambo lililozua wasiwasi kuhusu aliko.

Rafikize walisema Ayieko alitarajiwa kuhudhuria hafla nyingine mjini Kakamega siku ya Jumamosi, Oktoba 19, lakini hakufika.

Baadhi ya marafiki zake na wanafamilia wanasema walikisia kwamba kutoweka kwa Ayieko kunaweza kuhusishwa na majukumu yake kama Meneja wa Rasilimali ya Watu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved