logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mshukiwa mkuu wa uhalifu atiwa mbaroni Buuri Mashariki - Meru

Juhudi za polisi Meru za zaa matunda baada ya mzee mhalifu ambaye vamekuwa akiwahangaisha wakaazi Buuri Mashariki kutiwa mbaroni

image
na jacob kimanthi

Habari25 October 2024 - 12:48

Muhtasari


  • Mshukiwa wa uhalifu Meru katika eneo la Buuri Mashariki atiwa mbaroni huku akisubiri kuwasilishwa mahakani.
  • Mshukiwa alifumaniwa na polisi katika maficho yake baada ya polisi kudokezewa mahali alikokuwa akijificha.





Maafisa wa polisi katika neneo la Buuri mashaririki wamnasa mshukiwa mkuu wa wizi wa kidindia katika eneo hilo na kuweka maisha ya waakazi hatarini.Fredrick John Mwenda ambaye amekuwa akiwaangaisha wakaazi eneo hilo ametiwa mbaroni kufuatia juhudi za askari polisi.

Kutokana na lalama za wakaazi wa eneo hilo,ambao wamekuwa wakipiga ripoti kwa polisi,polisi walichukua hatua ya kuvamia makaazi ya Mwenda,ambako alikuwa amejificha baada ya kudokezewa mahali alikokuwa amejificha baada ya msako mkali kuendeshwa na polisi.Mwenda, alipatikana katika maficho yake yaliyoko katika kijiji cha Maili Tano,katika lokesheni ya Ruiri Rwarera.

Kutokana na msako huo,polisi walipata bunduki ambayo ilikuwa imeibiwa pamoja na risasi.Hii inajiri hivi karibuni baada ya visa vingi vya usalama duni kushuhudiwa katika kaunti hii.

Kukamatwa kwa mshukiwa huyu tishio,kunaonyesha jitihada za polisi kuendeleza isalama katika maeneo ambayo yamekumbwa na utomvu wa usalama kama kaunti hiyo ya Meru.

Visa vya utomvu wa usalama vimekuwa vikishuhudiwa kwa wingi tangia kuwepo kwea maandamano ya kuypinga mswada wa kifedha mwaka huu huku maandamano hayo yakiongozwa na kundi la Gen Z.

Aidha, kwa sasa nafasi ya waziri wa usalama wa ndani bado iko wazi baada ya waziri aliyekuwa katika nafasi hiyo, Kithure Kindiki kupendekezwa awe naibu rais baadab ya aliyekuwa naibu rais kubanduliwa mamalakani licha yakuwa kesi bado haijaweza kutamatika na kupata uamuzi wa kutua.

Mwenda sasa atazuiliwa huku akisubiri kuwasilishwa mahakamani huku siku bado ikiwa haijatangazwa rasmi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved