Mwizi mmoja kati ya genge la wezi saba apigwa risasi na kufa hapo kwa hapo baada ya kufumaniwa wakiharibu transfoma ndiposa waibe katika eneo la Kang'oki ,iliyoko Thika kaunti ya Kiambu.
Tukio hilo lilitokea mapema leo asubuhi na kuona juhudi za polisi katika eneo hilo la Thika walikuwa ange kabisa kwani genge hilo lilikuwa lishaa kata usambazaji wa umeme katika eneo hilo ili kutekeleza uhalifu huo.
Akidhibitisha taarifa hizi afisa mkuu wa polisi katika eneo la Thika, Lawrence Muchangi,ni kwamba genge hilo lilifumaniwa na polisi hawa jambo ambalo lilifuatisha mfarakano na mvutano baina ya polisi na wezi hao na ambapoi mwizi huyon alipigwa risasi na kufariki hapo kwa hapo na wengine kupata majeraha lakini kutorokea kusiko julikana.
Muchangi aliwahimiza wakaazi wa eneo hilo hususan madaktari wa vitongojini kupiga ripoti endapo wataona mtu yeyote ambaye atakuwa akihitaji huduma zozote za matibabu kutokana na risasi kwani itakuwa njia moja ya kurahisisha kupatikana kwao.
Aidha waliotoroka kwa sasa polisi wamo mbioni kutafuta waliko ndiposa kukomesha uhalifu huo na kukumbana na adhabu kali ya kisheria.
Kwa mujibu wa Dominic Thuo, ambaye ni afisa mkuu wa usalama kwenye shirika la usambazaji umeme Kenya Power, maeneo ya Kaskazini mashariki alidokeza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikipitia changamoto si haba za wizi wa transfoma,huku transfoma 25 zikiibiwa Kiambu kwa kipindi cha miezi sita, na kusababisha hasara ya takriban shilingi milioni 25.
Kufuatia juhudi za polisi kwa safari ya kukabiliana na wizi wa transfoma ili kuukomesha,ni jambo ambalo limewatia wengi matumaini hasa wakaazi wa eneo hilo vile vile wakitakiwa kuwa ange na kuripoti kisa chochote cha kaliba hile ndiposa hatua kuchukuliwa.Visa hivi vimekuwa vikiendelea kukidhiri katika eneo hilo na kukua kwa kasi.