Karibia wanawake na wasichana mia moja wamepoteza maisha yao kwa kuuawa kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita.Hii ni kutokana na taarifa ambazo zilitolewa na polisi huku visa vingi vikiendelea kushuhudiwa hapa nchini.
Aidha,mashirika ya utetezi wa haki za kibinadamu zilimtaka rais Dr. Wiliam Ruto kutangaza mauaji ya wanawake kama janga la kitaifa.
Kulingana na kitengo cha idara ya polisi ya kitaifa ,pamoja na idara ya uchunguzi wa jinai DCI walisema kuwa visa vya mauaji haya ya kinyama yamekuwa yakiongeza kwa sasa miaka miwili na wakatoa ahadi ya kutatua changamoto hiyo.
Vile vile polisi walisema kuwa wahusika wakuu wanafaa kuongezewa adhabu kwani kwani kumekuwepo na kutoadilika kwa wahusika wa mauaji.
Aidha, mauaji haya kwa wanawake yamekuwa yakitekelezwa na mashirika ya ulinzi pamoja na walinzi binafsi wa kaunti kwa viongozi na kutochukuliwa hatua sawia huku ikiweka hatarini usalama wa wanawake pamoja na wasichana.
"Kwa kipindi cha miezi mitatu pekee,taifa limeweza kuandikisha takriban visa 97 kwa mauaji ya wanawake" alisema naibu inspekta generali wa polisi Eliud Langat.
Vile vile Langat alisema kuwa mtindo huu ni ambao umeweza kuinua kope kwa kitengo cha usalama na ni lazima hatua zichukuliwe ndiposa kukomesha hulka hii.
"Tatizo hili limekuwa linaenea kwa haraka sana,na ipo haja ya kutafuta suluhu na ushirikiano ndiposa kukomesha tatizo la dhuluma za kininsia miongoni mwa wanajami"
Anne Wang’ombe akizungumza alisema kuwa ongezeko la visa hivi wanajamii ambao hawapigi ripoti kwa polisi pindi visa hivi vinavyofanyika licha ya kujua wahusika.
Kwa hakika mauaji ya wanawake yamekidhiri humu nchini na sasa linafaa kutangazwa kama janga la kitaifa huku serikali ikiombwa ifanye juhudi aghalabu kokomesha visa hivi na kuweka maisha ya wanawake kwenye usalama.
"Tangaza mauaji ya wanawake kama janga la kitaifa,tunafaa kuchukua visa vya mauaji ya wanawake kama tatizo kubwa" Janet Onyango ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa FIDA alisema.
Kulingana na takwimu kutoka kituo cha data cha African Data Hub,visa vya mauaji ya wanawake zimekuwa zikiongezeka kila mwaka, huku mwaka jana visa 75 zikirekodiwa.
Visa hivi kulingana na polisi,huenda vikawa tishio kwa usalama wa wanawake na wasichana.Aidha,pilisi ilisema kuwa wanajaribu kukabiliana na visa vilivyoripotiwa kwa hatua ya kisheria.
Kwa visa hivi, bado polisi walisema bado wanaendelea kumtafuta mshukiwa wa mauaji ya Kware, Collins Jumaisi.