Kanisa la Kiangilikani la Kenya limesema kuwa linaunga mkono uwajibishaji kwa serikali kutoka kwa kanisa la Katoliki lililofanywa na baraza la maaskofu wa Kikatoliki wiki jana.
Katika taarifa yake kwa vyumba vya habari, Sapit alisema tabaka la kisiasa na wale walio serikalini wanahitaji kushuka kwa kile alichokiita ‘kutoka kwa farasi wao wa juu’, na badala yake kusikiliza kwa mara moja, badala ya kuonekana kuendeleza utamaduni wa kawaida wa kutokujali.
"Watawala hawahitaji mihadhara lakini huduma na ushiriki wa uaminifu. Tafadhali jikite katika kutoa uongozi kwa njia ya maana na kwanza ushughulikie maelfu ya matatizo ambayo yanaidhalilisha nchi,” Ole Sapit alisema.
Katika taarifa yake Sapit alidokeza kuwa mtindo mpya wa ufadhili wa chuo kikuu haujafanya kazi tangu kuasisiwa miezi kadhaa iliyopita.
"Vyuo vikuu vya umma vinafanya kazi kwa shida. Ucheleweshaji wa mara kwa mara wa kutoa ufadhili kwa wanafunzi umeendelea kudhoofisha uendeshaji bora wa shule za umma.”
Vile vile Askofu huyo mkuu, amelalamikia mageuzi yaliyofanywa kutoka kwa mfumo wa bima ya afya ya NHIF kuingia mamlaka ya afya ya jamii SHA, akisema kuwa Wakenya wanazidi kuteseka na mabadiliko hayo kwa kuwa mabadiliko hayo bado hayajakuwa laini.
Ole Sapit pia ameitaka serikali kuwajibikia visa vya kupotea kwa Wakenya kupitia kutekwa nyara bila sababu pamoja na mauaji ambayo hayajatatuliwa.
Sapit aliongeza kuwa Wakenya wanatatizika kulipa kodi, matatizo ya ukosefu wa ajira na mazingira duni ya biashara.
Ujumbe wa Ole Sapit unajiri baada ya viongozi wanaoegemea upande wa serikali kukashifu uwajibishaji wa werikali wa wazi kutoka kwa viongozi wa kidini nchini.
Aidha
Sapit amejitenga na habari katika vyombo vya habari kuwa kanisa la ACK
halikubaliani na maaskofu wa kanisa Katoliki katika kuwajibisha serikali
Alisema maaskofu wamezungumza mawazo ya Wakenya
na kueleza ukweli kwa uaminifu wa mambo yalivyo mashinani.