Mtu mmoja ameangamia katika ajali ya barabarani nchini Tanzania baada ya gari alimokuwa akisafiria kupoteza mwelekeo na kubingiria mara kadhaa barabarani.
Gari hilo lilikuwa sehemu ya msafara wa magari yaliyokuwa yamewabeba waombelezaji waliokuwa wakipeleka maiti ya jamaa mmoja aliyekufa katika mkasa wa jingo la kibiashara kuporomoka mtaani Kariakoo kwenye jiji la Dar es Salaam.
Akidhibitisha kisa cha ajali hiyo, kamishna msaidizi wa polisi wa mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga alisema kuwa watu wengine wawili akiwemo dereva walipata majeraha na sasa wanaendelea kupokea matibabu.
Kamishna msaidizi huyo wa polisi alisema kwamba ajali hiyo ilitokea wakati dereva wa gari lililofanya ajali alishindwa kulidhibiti wakati alikuwa analipita gari linguine. Taarifa ya polisi ilisema kwamba baada ya dereva kushindwa kudhibiti gari, aligonga kikingi na kupinduka hivyo kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi wawili akiwemo.
Gari lililofanya ajali lilikuwa sehemu ya magari matatu yaliyokuwa katika msafara wa kupeleka maiti katika mji wa Tunduma kwa ajili ya mazishi ya mhanga wa wa ghorofa iliyoporomoka Kariakoo.
Zaidi ya watu 13 walipoteza maisha katika mkasa wa kuporomoka
kwa ghorofa jijini Dar es Salaam wiki jana.