Waziri wa leba daktari Alfred Mutua amesema kuwa Wakenya waliopata fursa za ajira katika nchi za ughaibuni watafanyiwa mafunzo kabla ya kuondoka nchini kuelekea kwenye nchi za Falme za Kiarabu.
Katika ujumbe wawaziri huyo kwenye ukurasa wake wa X, Muttua amesema kwamba utengenezaji wa stakabadhi na mikataba ya wafanyakazi watakaoelekea nchini ya Qatar inaendelea vyema huku siku ya kuondoka kuelekea Qatar ikiwadia.
Kabla ya kuondoka nchini, waziri Mutua amesema kuwa Wakenya waliofaulu kufaidi nafasi hizo za ajira na ambao tayari wametia sahihi kwenye barua za kupokea kazi hizo, watafanyiwa mafunzo maalum jijini Nairobi katika jumba la KICC mnamo Jumamosi kuanzia saa mbili asubuhi.
Aidha waziri huyo amesema kwamba wafanayakazi ambao hawajatia sahihi zao kwenye barua za kazi ilhali walipata mtihani wa kuajiriwa, wametakiwa kufika katika sehemu ambazo wamearifiwa kupitia barua siku ya Jumatatu kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Hata hivyo, wale ambao hawajatia sahihi kwenye barua za kazi wametakiwa kutoripoti kwenye mafunzo ya Jumamosi.
Vile vile, wafanyakazi ambao hawajapokea ujumbe wa kuwataka kutia sahihi kwenye barua za nafasi ya kazi, amewashauri kuwa watulivu akisema kwamba barua zao bado zinashughulikiwa katika taifa la Qatar na majibu yangerejea katika siku chache.
Wakenya wanaopata nafasi za kazi, katika mafunzo yanayofanywa nchini kabla ya kuondoka huja baada ya sahihi kutiwa na vipimo vya afya kufanyiwa wafanyakazi wanaobahatika.
Hata hivyo, orodha ya Wakenya 72 waliofanikiwa kuchukuliwa kwa nafasi mabli mbali za kazi wametakiwa kufika KICC mnamo Jumatatu Disemba 2, ili kutia sahihi barua zao za nafasi ya kazi.
Wengi waliofanikiwa ni madereva, fundi wa bomba za maji,
fundi wa stima na nesi.