Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka amependekeza kuteuliwa kwa aliyekuwa Karani wa Jiji la Nairobi Philip Kisia kama mkurugenzi mkuu mpya wa muungano wa Azimio La Umoja One Kenya.
Kisia atachukua nafasi ya Raphael Tuju iwapo atafanikiwa kutinga nafasi hiyo.
Musyoka alimtaja Kisa kama kiongozi mwenye uzoefu mkubwa kwenye utumishi wa umma, uongozi wa sekta ya kibinafsi, na ushirikiano wa jamii, akimtaja kuwa na sifa za kipekee kuongoza Sekretarieti ya Azimio.
"Ninapendekeza Bw Philip Kisia ateuliwe kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Azimio La Umoja One Kenya Coalition Party kuchukua nafasi kutoka kwa Mhe. Raphael Tuju."
"Uzoefu mkubwa wa Bw Kisia katika utumishi wa umma, uongozi wa sekta ya kibinafsi, na ushirikiano wa jamii, unamfanya kuwa na sifa za kipekee za kuongoza Sekretarieti ya Azimio inapohamia Muungano unaojumuisha wote na unaoendelea," Musyoka alisema.
Kisia ameshikilia nyadhifa muhimu ikiwa ni pamoja na kuhudumu kama Karani wa Jiji la Halmashauri ya Jiji la Nairobi. Vile vile ametwaa umashuhuri katika duru za utawala na biashara nchini Kenya.
Musyoka pia alitoa shukrani kwa Zein Abubakar kwa utumishi wake wa kujitolea kama mkuu wa Sekretarieti yake ya Rais katika kipindi cha miezi sita iliyopita.
“Napenda kumshukuru Mhe. Zein Abubakar kwa kukubali kuongoza Sekretarieti yangu ya Rais kwa muda wa miezi sita iliyopita. Historia yake tajiri na iliyojaa kielimu pamoja na uharakati wa miaka mingi tayari imeboresha Timu yetu ya Watu inayokua,” Musyoka alisema.
Akiangalia siku zijazo, Musyoka alifichua mipango ya kufichua wanachama wa ziada wa timu yake, ambao wamejitolea kupinga udikteta na kurejesha demokrasia ya kikatiba nchini.