Mwanamume mwenye umri wa miaka 40 anahofia maisha yake siku chache baada ya kumaliza kuhudumia kifungo chake jela cha miaka minne kwa kukufuru.
Mubarak Bala alihukumiwa kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hatia na mahakama moja nchini Nigeria. Bala alikiri makossa yote kumi na manne aliyoshtakiwa nayo kuhusu chapisho alilobandika kwenye ukuasa wake wa mtandao wa Facebook.
Jamaa huyo mkama Mungu ambaye ni maarufu Zaidi nchini Nigeria anahofia usalama wake baada ya kumaliza kifungu jela na kuachiliwa huru. Kwa mujibu wa shirika la habari la kimataifa la BBC, Mubarak Bala alisema kuwa wasiwasi kuhusu usalama wa maisha upo kila wakati.
Jamaa huyo ambaye awali alikuwa mshiriki wa dini ya Kiislamu, alikana uwepo wa Mungu mwaka wa 2014.
Akieleza kuhusu jinsi maisha yake yalikuwa wakati akihudumia kifungo gerezani, Bala alisema kuwa kuna wakati alikuwa anahofia maisha yake kutoka kwa wafungwa wengine akilini akiwaza ikiwa angeliwahi kumaliza kifungo chake na kutoka gerezani akiwa hai.
Hofu ya Bala kwa mujibu wake ilitokana na kuwa jela ya mwanzoni alikokuwa anazuiliwa kaskazini mwa Nigeria ilikuwa na wafungwa wengi wa dini ya Kiislamu. Eneo hilo la mji wa Kano linatambulika kwa kuwa na wafuasi wengi la Kiislamu.
Mkosoaji huo wa kidini alijipata pabaya baada ya kundi la mawakili
kuwasilisha ripoti kwa polisi kuhusu ujumbe aliokuwa amechapisha kwenye mtandao
wa facebook.