MBUNGE WA KAPSERET Oscar Sudi amedokeza kwamba hata yeye siku za usoni huenda akajaribu karata yake katika kiti cha urais.
Akizungumza na rais
William Ruto mwishoni mwa juma wakati wa ziara yake ya maendeleo kwenye bonde
la ufa, Sudi alisema kwamba Kenya ni ya kila mtu na kila mtu ana uwezo wa kuwa
rais siku moja.
Mbunge huyo alikariri
maneno yake kwamba hata watu waruke juu vipi, bado rais Ruto hakuna mahali
ataenda, akionyesha Imani kuu kwamba Ruto atachaguliwa tena 2027.
Alitaja uvumi unaoenezwa
mitandaoni kwamba rais Ruto anachukiwa na Wakenya kuwa propaganda za watu wa
Nairobi tu.
“Si mnajua wale wakora
wa mitandao kule Nairobi, wanapiga kelele eti sijui Ruto Must Go sijui nini… mimi
niliwaambia waruke juu, waende chini au kando, Ruto hakuna mahali anaenda.”
“Wale wanajifanya
wakifikiria kwamba wao tu ndio lazima waongoze hii nchi. Hapana, hata Mluhya au
Mturkana anaweza ongoza. Mkenya yeyote ako nja uwezo wa kuongoza. Si hata mimi
mtanipatia urais siku nyingine?” Sudi aliuliza umati
uliokuwa unamshangilia.
Katika ziara hiyo, rais
Ruto pia alimtania mbunge huyo akimtaja kama injinia ambaye hajulikani ni wa
nini.
“Ooh,
tuko na huyu injinia. Sijui ni injinia wa nini lakini tu ni injinia tusema,
anaitwa Oscar Sudi. Nasikia zamani alikuwa area huku sasa amepelea uinjinia
mpaka umefika Eldoret. Ahsante sana,”
Ruto alisema akimtambulisha Sudi kwa umma kwa njia ya utani.
Kitembo cha Sudi katika Nyanja ya masomo
kimekuwa ni mjadala pevu kwa miaka mingi sasa humu nchini.
Mbunge huyo ambaye ni mtetezi mkali wa sera
za rais William Ruto alijipata kuwa gumzo la mitandaoni mwaka jana baada ya
kufichua kuzawadiwa shahada na chuo kimoja.
Sudi alifichua kwamba alivishwa joho na
shahada ya uzamili ya kiheshima na chuo cha Northeastern Christian wakati
alipoudhuria hafla ya kufuzu kwa mahafali katika chuo anuwai cha Eldoret.
Shahada hiyo ilivutia joto la kisiasi
kutoka kwa baadhi ya watu, hadi ikapelekea mamlaka inayosimamia elimu ya juu
CUE kuingilia kati na kutaka shahada hiyo kuchunguzwa na kufutiliwa mbali
ikiwezekana