ZAIDI ya wafungwa 170 waliohukumiwa kifo walisafirishwa kwa ndege kutoka mji mkuu wa Kongo hadi kwenye gereza lenye ulinzi mkali kaskazini mwa nchi ambako watanyongwa, mamlaka ya Kongo ilisema wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa mashirika ya Habari ya kifamaita, Sabini
kati ya wafungwa hao walisafirishwa siku ya Jumapili wiki jana, Waziri wa
Sheria wa Kongo Constant Mutamba alisema, akiongeza wafungwa wengine 102 ambao
tayari wamepelekwa katika gereza la Angenga katika jimbo la kaskazini la Mongala.
Vijana hao wa kati ya miaka 18-35 wamepatikana na
hatia ya wizi wa kutumia silaha na wanajulikana kama "Kulunas" au
"majambazi wa mijini."
Wana umri wa kati ya miaka 18 na 35, Mutamba alisema
katika taarifa. Hakusema ni lini mauaji yatafanyika.
Baadhi wamekaribisha hatua hiyo kama njia ya
kurejesha utulivu na usalama katika miji, huku wengine wakiwa na wasiwasi
kuhusu hatari za unyanyasaji na ukiukaji wa haki za binadamu.
“Tunakaribisha
uamuzi huu wa waziri kwa sababu utasaidia kukomesha uhalifu wa mijini. Kuanzia
saa 8 mchana. kuendelea, huwezi kuzunguka kwa uhuru kwa sababu unaogopa
kukutana na Kuluna,” alisema Fiston Kakule, mkazi wa mji
wa mashariki wa Goma.
Espoir Muhinuka, mwanaharakati wa haki za binadamu,
alionya juu ya uwezekano wa kunyongwa bila ya mahakama na kutoa wito wa
kuheshimiwa kwa taratibu za mahakama na dhamana za kimsingi.
Anahofia kwamba shinikizo la kisiasa linaweza
kusababisha hukumu zisizo za haki na mauaji ya kiholela.
"Hali
nchini DRC ni ngumu na inahitaji mtazamo wa pande nyingi. Mapambano dhidi ya
magenge ya mijini lazima yaende sambamba na juhudi za kupambana na umaskini,
ukosefu wa ajira na kutengwa na jamii, mambo ambayo mara nyingi yanachangia
uhalifu,” alisema.
Kongo ilifuta hukumu ya kifo mwaka 1981, lakini
ilirejeshwa mwaka wa 2006. Unyongaji wa mwisho ulifanyika mwaka wa 2003.
Mnamo Machi 2024, serikali ya Kongo ilitangaza kuanza
tena kwa adhabu ya kifo katika kesi za uhaini zilizofanywa na wanajeshi.
Mnamo Mei, wanajeshi wanane walihukumiwa kifo, na
mnamo Julai, wanajeshi 25 walitiwa hatiani kwa makosa kama hayo. Hakuna
anayejulikana kunyongwa.