Polisi katika Kaunti ndogo ya Rangwe, Kaunti ya Homa bay wamemkamata Askofu wa kanisa la mtaa katika kijiji cha Ndiru katika eneo ndogo la Kokoko kwa madai ya kufanya ngono na bintiye wa kumzaa.
Askofu wa kanisa la mtaa eneo la Ndiru ndani ya Wadi ya Kagan alikamatwa na maafisa kutoka kituo cha polisi cha Ndiru kufuatia malalamishi kutoka kwa wananchi.
Kulingana na wenyeji, kasisi huyo alibanwa na mmoja wa wanakijiji akifanya mapenzi na bintiye ambaye ni mama wa watoto watatu.
Kamanda wa polisi wa Kaunti Ndogo ya Rangwe Magdaline Chebet anasema walipata taarifa kutoka kwa umma kwamba askofu huyo amekuwa akifanya ngono na bintiye ambaye alikuwa ameolewa na kutengwa na mume wake.
Chebet anasema kuwa maafisa kutoka kituo cha polisi cha Ndiru wakiongozwa na OCS walienda kwa makasisi na kumkamata baada ya ghasia za umma.
Askofu huyo alipelekwa katika kituo cha polisi cha Ndiru ambako anazuiliwa hadi uchunguzi ukiendelea.
Binti ya askofu huyo alihojiwa baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kuachiliwa.