
MBUNGE wa Homa Bay mjini Peter Kaluma ameomba desturi ya kutahiri wanaume nchini Kenya kupigwa marufuku akisema kwamba suala hilo halina umuhimu wowote katika maisha na mwili wa mwanamume.
Kupitia ukurasa wake wa X, Kaluma alisema kwamba suala la
kutahiri watoto wa kiume lilikuwa linafanywa tu na Abraham kwenye Biblia enzi za
zamani kwa sababu yeye alikuwa anaishi jangwani pasipo na maji.
Mbunge huyo alisema kwamba kutahiri wanaume ni sawa na
kuhujumu haki zao za kiume, akidai kwamba ni desturi isiyo na maana yoyote.
Kaluma alisema kwamba hakuna mnyama wa kiume hata mmoja ambaye
anatahiri isipokuwa tu mwanadamu, akitolea mfano kwamba hata punda hawatahiri
na wanaishi sawa tu!
“Acha kutahiriwa. Tohara
ni kukata wanaume. Punda hawatahiri. Wanyama wote hutahiriwa isipokuwa wanadamu
wachache ambao wamedanganywa kwamba wao ni wajukuu wa Abrahamu, mtu aliyeishi
jangwani bila maji!” Kaluma alisema.
Licha ya maoni yake kuonekana kuwa na maana, baadhi ya
watumizi wa X walionekana kukinzana naye, wengine wakisema kuwa mwanamume
kutahiriwa humdumishia usafi wan yeti yake.
Haya hapa ni baadhi ya maoni;
@nyawade_rodgers: ‘Hapa uko pekee yako. Tohara ni jambo bora
zaidi ambalo mwanaume anaweza kujifanyia mwenyewe.”
@__Munguti: “Je, unasema Bwana alikuwa mwendawazimu
alipoamuru kutahiriwa? Hivi majuzi, inaonekana kama umetweet ili kugusa ego
yako. Ikiwa hujakatwa, hiyo ni biashara yako-waache wale wanaotaka wafanye
mambo yao. Jiwekee!”
@justinawamae: “Nitawaongoza wanawake kupinga maoni yako.”
@mtume_tyson: “Unapoanza kwenda kinyume na neno la Bwana,
maana yake umepoteza mwelekeo... unaelekea uharibifu.”
@MaishmainaB: “Tohara ya wanaume sio tu kukatwa, ni mengi
yanayoambatana na.haki ya kupita.kama jamii hufanyi mazoezi waache wanaofanya
hivyo.unachoamini ndicho unachopata.”
@didacushill: “Ngozi ya mbele ndiyo sababu ya watu wengi
kuwasiliana na VVU. Wakati wa kujamiiana, ngozi ya mbele inasukumwa nyuma ili
kufichua glans ya uume. chini ya msukumo mkali, msukumo huu husababisha machozi
kwenye sehemu ya govi ya kugusana na glans. Hii inaweka wazi mwathirika kwa
maambukizo kwa nafasi ya 80%. Acheni uwongo kwa luos, watakufa kama panya.”