logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Idara ya mahakama yatoa taarifa jamaa kujichoma nje ya mahakama ya upeo

Ikielezea shughuli za mtu huyo hadi kufikia tukio hilo, Mahakama ilifichua kuwa inasadikiwa alikuwa akipinga kucheleweshwa kwa haki na alikuwa na petroli ambayo aliitumia kujichoma moto.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Habari12 March 2025 - 10:04

Muhtasari


  • Kisa sawia na hicho kilishuhudiwa nchini Uganda wiki 2 zilizopita wakati mwanamume alijimwagia petroli na kujiwasha moto nje ya bunge la taifa hilo.
  • Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, mwanamume huyo alijichocha kwa kulalamikia chama tawala cha NUP kumpuuza.
  • Japo alikimbizwa hospitalini, alithibitishwa kuaga dunia mapema wiki hii kutokana na ukali wa majeraha aliyopata.

Mahakama ya upeo

IDARA ya mahakama nchini Kenya Jumanne jioni ilitoa taarifa kufuatia kisa cha mwanamume wa umri wa makamo kujiteketeza nje ya mahakama ya upeo.

Katika taarifa yao, Idara ya Mahakama ilithibitisha kuwa mwanamume huyo ambaye alipata majeraha mabaya katika tukio hilo la kushangaza, atahojiwa na polisi ili kubaini sababu za kitendo chake hicho. 

Ikielezea shughuli za mtu huyo hadi kufikia tukio hilo, Mahakama ilifichua kuwa inasadikiwa alikuwa akipinga kucheleweshwa kwa haki na alikuwa na petroli ambayo aliitumia kujichoma moto.

"Leo saa 9:30 asubuhi, mwanamume ambaye bado hajatambulika kwa njia kamili, alipokuwa akitembea kando ya City Hall Way, alisimama nje ya jengo la Mahakama ya Juu Zaidi. Alikuwa amebeba baadhi ya nyaraka na chupa yenye kimiminika,” Mahakama ilisema Jumanne jioni.

“Akiwa amesimama kwenye kando ya barabara, aliweka nyaraka hizo chini, akajimwagia maji yanayosadikiwa kuwa ya petroli, kisha akachomoa njiti na kujichoma moto,” waliongeza. 

Maafisa wa polisi wanaolinda Mahakama ya Juu waliitikia kwa haraka hali hiyo, na kumuokoa mwanamume huyo kwa kuzima moto huo. 

Juhudi za pamoja za Serikali ya Kaunti ya Nairobi na maafisa hao zilimwona akikimbizwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta. 

Kuhusiana na malalamiko ya mwanamume huyo na mahakama, Mahakama ilisema kwamba itachunguza suala hilo zaidi ili kubaini matatizo yake ya msingi.

Kisa sawia na hicho kilishuhudiwa nchini Uganda wiki 2 zilizopita wakati mwanamume alijimwagia petroli na kujiwasha moto nje ya bunge la taifa hilo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, mwanamume huyo alijichocha kwa kulalamikia chama tawala cha NUP kumpuuza.

Japo alikimbizwa hospitalini, alithibitishwa kuaga dunia mapema wiki hii kutokana na ukali wa majeraha aliyopata.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved