
Polisi huko Eldama Ravine wanamsaka mwanamume mmoja baada ya mke wake wa zamani mwenye umri wa miaka 32 kuuawa baada ya kuhama.
Katika taarifa ya Jumanne, Machi 25, 2025, Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ilisema mwili wa mwanamke huyo ulipatikana nje ya nyumba ya mpenzi wake wa sasa mnamo Jumatatu, Machi 24, 2025.
Mwili huo ulikuwa na majeraha makubwa kichwani.
"Polisi wa Eldama Ravine, kaunti ya Baringo wanachunguza mauaji ya kutisha ya mwanamke mwenye umri wa miaka 32, anayeaminika kudhulumiwa na kuuawa na aliyekuwa mume wake ambaye alikasirishwa na kusukumana na mwanamume mwingine," DCI ilisema.
"Tukio hilo la kuhuzunisha liliripotiwa na Chifu wa eneo la Saos Bi Judith Chebon jana usiku, baada ya kupata maiti ya mwanamke huyo ikiwa imetapakaa nje ya nyumba ya kupanga ya mpenzi wake wa sasa ikiwa na majeraha makubwa kichwani."
Maafisa wa upelelezi kutoka DCI Koibatek wameanza uchunguzi, na mhusika Alex Kimeli Ng’elel (mume), ambaye tangu wakati huo amekimbilia mafichoni anasakwa.
"Majirani walioshuhudia tukio hilo la kuogofya kwa hasira walibaini kuwa walimwona mwathiriwa mara ya mwisho akielekea nyumbani kwa mpenzi huyo muda wa saa nane mchana, lakini mwili wake ulipatikana saa tisa usiku ukiwa umelowa damu kwenye boma," DCI ilisema.