
NAIROBI, KENYA, Julai 28, 2025 — Mwakilishi wa Wadi ya Kileleshwa, Robert Alai, ameibua tuhuma nzito dhidi ya wafuasi wa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, akidai kuwa tukio la vurugu lililotokea Murang’a lilipangwa kwa ajili ya kujinufaisha kisiasa.
Katika tukio lililotokea siku ya Jumapili, baada ya ibada katika Kanisa la AIPCA Christ the King Church eneo la Kahuro, Kigumo, wanasiasa wanaomuunga mkono Naibu Rais Rigathi Gachagua, akiwemo Seneta wa Nyandarua John Methu, walidai kuvamiwa na polisi na kukumbwa na mashambulizi ya mabomu ya machozi na risasi za moto.
Hata hivyo, kauli ya Mwakilishi Wadi Kileleshwa Robert Alai imegeuza kabisa mwelekeo wa mjadala wa kisiasa nchini. Kupitia mitandao ya kijamii, Alai alikanusha madai hayo na kusema tukio hilo “halikuwa halisi bali la kupangwa.”
“Risasi hii imepangwa. Risasi ya moto haiwezi kutoka pamoja na ganda lake. Ganda huanguka karibu na bunduki, haliwezi kusafiri pamoja na risasi hadi kwenye gari,” aliandika Alai.
Hii risasi imepangwa. Risasi ya moto haiwezi kuwa imechomoza pamoja na casing. Casing huanguka karibu na bunduki, si kusafiri na projectile hadi kwenye gari,” aliandika Alai, akiongeza kuwa picha iliyotumika kusambaza taarifa hiyo ilikusudiwa “kuongoza wananchi kiakili.”
“Hawa watu wanajua mbinu za propaganda. Wanatumia picha za kuigiza na kutengeneza hofu ili kuvutia huruma ya kisiasa. Ni mbinu za kuchosha,” aliongeza kwenye chapisho jingine.
“Ni aibu kuona viongozi wanapanga matukio ya vurugu ili kuhalalisha siasa zao chafu. Hii siyo njia ya kuelekea 2027, ni njia ya kusambaratisha taifa,” alisema Alai katika mahojiano ya redio baadaye jioni.
Kwa upande wao, viongozi wa DCP waliendelea kushikilia kuwa walivamiwa na maafisa wa polisi kwa nia ya kuwazima kisiasa.
Seneta Methu alisema kuwa walilazimika kutoroka kwa miguu baada ya msafara wao kushambuliwa kwa mabomu na risasi.
“Polisi waliokuwa na maagizo maalum walitushambulia Ngonda, Kigumo, na kutumia risasi za moto dhidi ya msafara wetu. Tulikimbia kwa miguu, ilikuwa ni kifo au kukimbia,” alisema Methu.
Naibu Rais Rigathi Gachagua, kwa hasira, alitoa taarifa akilaani tukio hilo na kuitaja serikali ya Rais Ruto kuwa “ya kidikteta” na kutumia vyombo vya dola kwa ukatili.