Tanzia!Mwanahabari wa runinga ya KBC Badi Muhsin ameaga dunia

Muhtasari
  • Mwanahabari wa runinga ya KBC Badi Muhsin ameaga dunia
Badi Muhsin
Image: Twitter

Mtangazaji mkongwe wa habari za kiswahili katika runinga ya KBC Badi Muhsin ameaga dunia.

Familia ilisema aliaga baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kulingana na kaka yake Hafidh Muhsin, mwanahabari  huyo mashuhuri alikuwa sawa na hata walilkula chakula cha mchana pamoja na hata kuenda katika chumba chake cha hoteli ambapo aliaga dunia.

Aliripotiwa kujisikia vibaya mchana muda mfupi baada ya kula chakula cha mchana.

Badi ameaga dunia akiwa na miaka 67.

Kutoka kwetu wanajambo Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.