logo

NOW ON AIR

Listen in Live

City Hall yateketezwa huku maandamano yakichacha

Waandamanaji jijini Nairobi wamechoma Ikulu ya Jiji.

image
na Radio Jambo

Habari25 June 2024 - 13:22

Muhtasari


    City Hall  yawaka moto huku maandamano ya kupinga Muswada wa Sheria ya Fedha yakizidi

    Waandamanaji jijini Nairobi wamechoma Ikulu ya Jiji.

    Video zilizoonekana na Radiojambo zilionyesha moshi mkubwa ukitoka kwenye jengo hilo.

    Maafisa wa polisi walionekana wakizunguka jengo hilo.

    Haya yanajiri saa chache baada ya waandamanji kuingia bunge na kuharibu baadi ya bidhaa katika jengo hilo.

    Picha za Televisheni za moja kwa moja zinaonesha sehemu ya bunge ikiwa imeharibiwa vibaya.

    Madirisha na viti vinaweza kuonekana vimevunjwa huku polisi wakiendelea kuwasukuma nje waandamanaji waliolifikia jengo hilo.

     

     


    RADIO JAMBO FREQUENCIES

    Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


    logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved