Ndege nyepesi imeanguka katika eneo la Kwachocha huko Malindi kando ya barabara kuu ya Malindi-Mombasa.
Picha za video zilizosambazwa mtandaoni zilionyesha sehemu za ndege hiyo zikiwa barabarani huku sehemu yake ikiwa inawaka moto, jambo linaloashiria kuwa ililipuka na kuwaka moto.
Kulingana na mashuhuda, inadaiwa kuwa ndege hiyi ilianguka mahali kulikuwa na pikipiki.
Kufikia kuchapisha taarifa hii, kiwango kamili cha athari ya ajali hiyo ilikuwa bado haijabainika.
Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo itatolewa.