Chebukati alifariki akipokea matibabu katika hospitali moja mjini Nairobi.
Chebukati alikuwa melazwa katika hospitali moja jijini Nairobi ambapo amekuwa akitibiwa kwa takriban wiki moja.
Duru kutoka hospitali zilikuwa zimesema kwamba alikuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo.
Chebukati alihudumu kama mwenyekiti wa IEBC kwa muhula mzima wa miaka sita na alistaafu Januari 2023.
Aliongoza chaguzi za 2017 na 2022.