logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Isaac Mutuma aapishwa kama gavana wa nne wa kaunti ya Meru baada ya Mwangaza kubanduliwa

Aliyekuwa Naibu Gavana katika kaunti yaMeru Isaac Mutuma ameapishwa rasmi kama Gavana wa kauti hiyo

image
na Japheth Nyongesa

Hivi Punde17 March 2025 - 10:54

Muhtasari


  • Jaji alithibitisha kuwa Mwangaza alipewa haki ya kusikilizwa na kutupilia mbali ombi lake la kubatilisha notisi ya gazeti la serikali inayothibitisha kuondolewa kwake.
  • Hii ni mara ya tatu kwa Mwangaza kufika katika Bunge la Seneti tangu alipochaguliwa kuingia madarakani Agosti 2022..

Isaac Mutuma, New Meru Governor

Aliyekuwa Naibu Gavana katika kaunti yaMeru Isaac Mutuma ameapishwa rasmi kama Gavana wa kauti hiyo siku ya leo 17.

Kuapishwa kwa Mutuma kumefanyika siku chake tu baada ya mahakamu kuu kuidhinishawa kuondolewa kwa aliyekuwa Gavana wa Kauniti hiyo Kawira Mwangaza baada ya kupitishwa na bunge la seneti.

Sherehe za kuapishwa  kwake zimefanyika katika uwanja vya Mwendantu mjini Meru.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na waziri wa maji Eric Muga, PS Patrick Kiburi, Naibu Gavana wa Laikipia Reuben Kamuri miongoni mwa viongozi wengine.

Katika hukumu iliyotolewa Ijumaa, Machi 14, Jaji Bahati Mwamuye aliamua kwamba ombi la kupinga kuondolewa kwa Mwangaza halikufikia kizingiti cha kisheria cha kubatilisha uamuzi wa Seneti.

Jaji alithibitisha kuwa Mwangaza alipewa haki ya kusikilizwa na kutupilia mbali ombi lake la kubatilisha notisi ya gazeti la serikali inayothibitisha kuondolewa kwake.

Mutuma alichaguliwa kuwa naibu gavana wa Meru katika uchaguzi wa 2022 pamoja na Mwangaza bila kudhaminiwa na chama chochote cha kisiasa.

Waliibuka na ushindi, wakiwabwaga waliokuwa vigogo wa kisiasa huko Meru akiwemo aliyekuwa gavana Kiraitu Murungi na mtangulizi wake Peter Munya.

Kabla ya kuchaguliwa kwake, Mutuma alihudumu kama afisa mwandamizi katika Huduma ya Magereza ya Kenya na alifanya kazi kama Mchungaji katika Makanisa ya Methodisti ya Kenya.

Ana Stashahada ya Juu katika Saikolojia ya Uchunguzi "Criminology" kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Kenya katika Haki ya Jinai, pamoja na Shahada ya Uzamili katika Theolojia kutoka Chuo Kikuu cha Kenya Methodist.

 Maseneta 26, mnamo Agosti 21, 2024, walipiga kura kuunga mkono shitaka la kwanza la ukiukaji mkubwa wa katiba na sheria zingine. Maseneta 14 wakikosa kuwepo kwenye kikao huku wanne wakipiga kura ya kumpendelea.

Katika shtaka la pili la utovu wa nidhamu, maseneta 26 walipiga kura kuunga mkono kuondolewa kwake madarakani, wawili dhidi ya, huku wengine 14 wakikwepa

Maseneta 27 waliidhinisha mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi, mmoja alipiga kura dhidi yake, na 14 wakikosekana. 

Hii ni mara ya tatu kwa Mwangaza kufika katika Bunge la Seneti tangu alipochaguliwa kuingia madarakani Agosti 2022.

Kesi ya kwanza ya mashtaka ilisikilizwa na kuamuliwa na kamati, lakini ya pili na ya tatu ilienda kwa njia ya jumla kwenye seneti.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved