logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Papa Francis afariki dunia Jumatatu ya Pasaka

Alikuwa na umri wa miaka 88 wakati wa kifo chake

image
na Tony Mballa

Hivi Punde21 April 2025 - 11:10

Muhtasari


  • Papa, ambaye sehemu ya pafu moja ilitolewa akiwa na umri wa miaka 20 na alikuwa amepambana na matatizo ya afya kwa miaka mingi, alilazwa Gemelli tarehe 14 Februari.
  • Katika miaka ya hivi majuzi alilazwa hospitalini mara kadhaa katika Gemelli ambapo alitibiwa katika chumba cha orofa ya 10 kilichohifadhiwa mapapa pekee.

Papa Francis alifariki dunia mjini Vatican Jumatatu, akiwa na umri wa miaka 88.

Papa huyo raia wa Argentina hivi majuzi alitumia wiki tano katika hospitali akipambana na nimonia.

Francis alihudumu kama papa kwa takriban miaka 12, baada ya kuchaguliwa kwake tarehe Machine 13, 2013 kufuatia kujiuzulu kwa mshtuko kwa mtangulizi wake Benedict XVI.

Papa, ambaye sehemu ya pafu moja ilitolewa akiwa na umri wa miaka 20 na alikuwa amepambana na matatizo ya afya kwa miaka mingi, alilazwa Gemelli tarehe 14 Februari.

Katika miaka ya hivi majuzi alilazwa hospitalini mara kadhaa katika Gemelli ambapo alitibiwa katika chumba cha orofa ya 10 kilichohifadhiwa mapapa pekee.

Kifo cha papa kinakuja wakati wa Mwaka wa Yubile wa Vatikani, tukio kuu la kidini linalofanyika Roma kila robo karne.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved