BURIANI CHAMP

"Tunampenda kijana wetu mzuri na tutampeza milele" Biden aomboleza mbwa wake kwa ujumbe maalum

Amesema kuwa 'Champ', kama alivyoitwa mbwa yule, hakuwa mbwa wa kawaida tu ila alikuwa mwenzao waliyempenda sana

Muhtasari

•"Amekuwa mwenzetu daima kwa kipindi cha miaka kumi na mitatu iliyopita na alipendwa na familia yote ya Biden. Hata nguvu yake ilipoendelea kudidimia miezi ya hivi karibuni, tulipoingia kwa nyumba alikuwa anajiinua huku akitingisha mkia na kutaka tumsugue sikio ama tumbo" Biden aliandika.

•Champ alikuwa mmoja kati ya mbwa wawili wa rais Biden wanaojulikana na alikuwa ndiye mkubwa kati ya mbwa hao wawili

Biden na mbwa wake 'Champ'
Biden na mbwa wake 'Champ'
Image: Hisani

"Nyoyo zetu ni nzito siku ya leo tunapowajulisha nyote kuwa mbwa wetu aina ya German Shepherd tuliyempenda zaidi ameaga kwa amani hapa nyumbani" ndio ujumbe ambao aliandika rais wa Marekani Joe Biden siku ya Jumamosi.

Rais Biden ameandika ujumbe maalum akimsfia na kuomboleza mbwa ambaye amekuwa akiishi na familia yake kwa kipindi cha miaka kumi na mitatu.

Amesema kuwa 'Champ', kama alivyoitwa mbwa yule, hakuwa mbwa wa kawaida tu ila alikuwa mwenzao waliyempenda sana.

"Amekuwa mwenzetu daima kwa kipindi cha miaka kumi na mitatu iliyopita na alipendwa na familia yote ya Biden. Hata nguvu yake ilipoendelea kudidimia miezi ya hivi karibuni, tulipoingia kwa nyumba alikuwa anajiinua huku akitingisha mkia na kutaka tumsugue sikio ama tumbo" Biden aliandika.

Champ
Champ
Image: Hisani

Amesema kuwa Champ alipendelea sana kuwa mahala popote ambapo walikuwa.

"Alipenda zaidi kujikunja kwenye miguu yetu mbele ya moto kila jioni, tuungana nasi kwenye mikutano ama kuota jua kwenye shamba la ikulu.  Kwenye siku zetu za furaha na  zile za huzuni, alikuwa hapo nasi, ni ngumu kueleza hisia fiche zilizo ndani ya nyoyo zetu kwa sasa. Tunampenda kijana wetu mzuri na tutampeza milele" aliandika rais Biden.

Champ alikuwa mmoja kati ya mbwa wawili wa rais Biden wanaojulikana . Alikuwa ndiye mkubwa kati ya mbwa hao wawili

Major ambaye ndiye mbwa wa pili wa Biden alizaliwa mwaka wa 2018.