logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mkuu wa majeshi aonya madaktari dhidi ya kutibu LGBTQ

"Kitu ambacho mbwa ukimpa chakula chini hawezi kufanya"

image
na Radio Jambo

Makala08 February 2023 - 08:53

Muhtasari


• Haiwezekani mtu anakuja na nepi zinavuja na anataka matibabu kwa sababu alifanya uamuzi kana kwamba hana akili - Jenerai huyo aisema.

Naibu kamanda wa majieshi ya ardhini nchini Uganda Meja jenerali Francis Takwira ametoa onyo kali dhidi ya wahudumu wa afya nchini humo wanaotoa huduma za matibabu kwa wanachama wa LGBTQ.

Meja Jenerali Takirwa alitoa kauli hiyo Jumapili wakati Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) lilipozindua na kukabidhi miradi tofauti kwa wakazi wa Wilaya ya Mbarara katika makao makuu ya Bwizibwera, jarida la Daily Monitor liliripoti.

“Msitumie vituo vyetu vya afya kuwatibu mashoga, mtu anakuja na nepi zinavuja na anataka matibabu kwa sababu alifanya uamuzi kana kwamba hana akili. Hapana. Hii ni nyingi sana na haikubaliki," Meja jenerali Takirwa alisema.

Alinukuliwa akisema kuwa vitendo hivyo ni vya aibu na havipaswi kukubalika.

“Mtu anakuja na kuanza kufanya vitendo hivyo vya aibu, visivyo vya asili, visivyo vya Kiafrika na wewe ukae kimya. Kitu ambacho mbwa ukimpa chakula chini hawezi kufanya lakini wewe mwenye akili unakula kwenye sahani unaweza kufanya, ni aibu. Mungu yuko karibu kuturekebisha, na mjiandae kufanya baadhi ya mazoea haya hata mbwa hawawezi kufanya, "alisema.

Jeshi hilo lilitoa hospitali iliyokamilika na bidhaa zote kwa jamii hiyo wakisema kwamba wao hata kama ni wanajeshi lakini asili yao ni kwa wanajamii ambao walisaidia katika ukombozi wa pili wakati Museveni alikuwa anaingia madarakani miaka Zaidi ya 30 iliyopita.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved