logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Brazil: Watu 14 wafariki katika ajali ya ndege huko Amazon

Uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha tukio hilo.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri17 September 2023 - 09:26

Muhtasari


  • Maafisa walisema wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo - abiria 12 na wafanyakazi wawili - walifariki katika ajali hiyo.

Watu 14 wamefariki katika ajali ya ndege kufuatia hali mbaya ya hewa katika eneo la Amazon nchini Brazil siku ya Jumamosi.

Ndege hiyo ndogo ya propela ilikuwa inakaribia mwisho wa safari yake ya kilomita 400 (maili 248) kati ya Manaus, mji mkuu wa jimbo la Amazonas, na mji wa mbali wa msitu wa Barcelos ilipoanguka.

Maafisa walisema wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo - abiria 12 na wafanyakazi wawili - walifariki katika ajali hiyo.

Uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha tukio hilo.

Waziri wa usalama wa jimbo la Amazonas Vinicius Almeida alisema taarifa za awali zilidokeza kwamba ndege hiyo ilianguka baada ya kupoteza mwelekeo wakati lipokuwa ikitua Barcelos.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved