logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Papa amtimua askofu anayepinga mabadiliko

Askofu huyo ameondolewa madarakani kufuatia uchunguzi katika Jimbo Katoliki la Tyler, huko Texas, Marekani .

image
na Samuel Maina

Habari12 November 2023 - 07:47

Muhtasari


  • •Askofu huyo ameondolewa madarakani kufuatia uchunguzi katika Jimbo Katoliki la Tyler, huko Texas, Marekani alilokuwa akiliongoza .
  • •Akofu Strickland ameshambulia hatua za Papa kutaka kubadili msimamo wa Ukatoliki katika masuala kadhaa ya kijamii ikiwemo kutoa mimba.

Papa Francis amemfuta kazi askofu Joseph Strickland, ambaye ni mkosoaji mkubwa aliyeibua maswali juu ya uongozi wa Papa katika Kanisa Katoliki.

Kwa mujibu wa taarifa ya Vatican, askofu huyo ameondolewa madarakani kufuatia uchunguzi katika Jimbo Katoliki la Tyler, huko Texas, Marekani alilokuwa akiliongoza .

Askofu Strickland ni mmoja kati ya sauti kinara katika tawi la uongozi wa Kanisa Katoliki nchini Marekani ambalo linapinga vikali mabadiliko yanayopigiwa chapuo na Papa.

Kuondolewa kwake kunakuja baada ya Papa kuzungumzia juu ya hali “ya kuwa nyuma” kifikra ya baadhi ya viongozi wa Kikatoliki nchini Marekani.

Askofu Strickland mara kadhaa ameshambulia hatua za Papa kutaka kubadili msimamo wa Ukatoliki katika masuala kadhaa ya kijamii ikiwemo kutoa mimba, haki za waliobadili jinsia na ndoa za jinsi moja.

Mwezi Julai mwaka huu, alionya kuwa mafunzo mengi ya Ukatoliki ambayo ni ya “ukweli wa msingi” yalikuwa yanapingwa, ikiwemo kile alichokiita majaribio ya “kudunisha” ndoa “kama ilivyoundwa na Mungu” baina ya mwanamume na mwanamke tu.

Askofu huyo pia amekosoa majaribio hayo aliyoyaita ya “kuvunja miiko” na kusema wanaoyapigia chapuo “wanapinga utambulisho wao wa kibailojia waliopewa na Mungu”.

Katika barua yake ya mwezi Julai, askofu Strickland amedai kuwa majaribio “kubadilisha visivyobadilika” yatasababisha mfarakano mkubwa ndani ya Kanisa. Na wale wanaotaka mabadiliko, ameonya kuwa “ndio hasa wanaofarakanisha [Kanisa]".

Askofu Strickland alikuwa chini ya uchunguzi wa Vatican na hapo awali alitupilia mbali uwezekano wa kujiuzulu, na katika barua ya wazi mwezi Septemba alimtaka Papa amfute kazi.

"Siwezi kujiuzulu kama Askofu wa Tyler kwa sababu kufanya hivyo itakuwa ninawatelekeza wana kondoo,” alisema..

Mwezi Julai mwaka huu, alionya kuwa mafunzo mengi ya Ukatoliki ambayo ni ya “ukweli wa msingi” yalikuwa yanapingwa, ikiwemo kile alichokiita majaribio ya “kudunisha” ndoa “kama ilivyoundwa na Mungu” baina ya mwanamume na mwanamke tu.

Askofu huyo pia amekosoa majaribio hayo aliyoyaita ya “kuvunja miiko” na kusema wanaoyapigia chapuo “wanapinga utambulisho wao wa kibailojia waliopewa na Mungu”.

Katika barua yake ya mwezi Julai, askofu Strickland amedai kuwa majaribio “kubadilisha visivyobadilika” kutasababisha mfarakano mkubwa ndani ya Kanisa. Na wale wanaotaka mabadiliko, ameonya kuwa ndio “ndio hasa wanaofarakanisha [Kanisa]".

Askofu Strickland alikuwa chini ya uchunguzi wa Vatican na hapo awali alitupilia mbali uwezekano wa kujiuzulu, na katika barua ya wazi mwezi Septemba alimtaka Papa amfute kazi.

Mwezi Oktoba Papa alisema kuwa Kanisa linaweza kukubali kubariki wanandoa wa jinsi moja, huku akiwaeleza makardinali kuwa "hatuwezi kuwa majaji ambao tunachofanya ni kukana, kukataa na kutenga tu".

Akizungunza katika mkutano wa Siku ya Vijana Duniani jijini Lisbon Papa alisema kuwa mgando wa fikra wa baadhi ya watu “hauna manufaa”.

"Kwa kufanya hivyo unapoteza utamaduni halisi na utategemea itikadi ili kuungwa mkono. Kwa maana nyingine, itikadi inachukua nafasi ya imani,” aliongeza kusema.

Mabadiliko ya tabianchi pia imekuwa ni moja ya ajenda kuu ya utawala wa Papa Francis - ambapo mwaka 2015 alitoa chapisho muhimu kuhusu mazingira ambalo lilionya kuwa dunia ilikuwa inaelekea hatua mbaya zaidi kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Papa pia amewashutumu vikali wale wote wanaokanusha mabadiliko ya tabianchi na anatazamiwa kuwa katika mkutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa wa COP28) baadae mwezi huu huko Dubai.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Papa kuhudhuria toka mikutano hiyo ianzishwe mwaka 1995.

Vatican imesema kuwa Jimbo la Tyler kwa sasa litaongozwa kwa mpito na Askofu Joe Vasquez wa Jimbo la Austin.

Kwa mujibu wa Vatican, uamuzi wa kumfukuza umefikiwa baada ya “ziara ya kitume katika Jimbo la Tyler iliyoagizwa na Papa mwezi Juni".

Vyombo vya habari vya Kikatoliki vinaeleza kuwa uchunguzi huo pia uliangazia masuala ya kifedha katika jimbo hilo.

Askofu Strickland, 65, aliteuliwa kuwa askofu mwaka 2012, wakati wa Papa Benedikto XVI.

Hatua hii inafuatia hatua mahususi zinazochukuliwa na Papa ili kulifanya Kanisa Katoliki kuendana na wakati kwenye utawala wake.

Siku ya Alhamisi, Vatican ilitangaza kuwa watu waliobadili jinsia wanaweza kubatizwa katika Kanisa Katoliki ilimradi kwa kwa kufanya hivyo hakutazua kashfa ama “mchafuko”.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved